Wednesday, August 8, 2012

J Mutahangarwa: the first Tanzanian with a medical license

Joseph Rutakolezibwa Mutahangarwa was born in a chiefly family in Kiziba in the Kagera region. He was the first Tanganyikan to complete the medical course at Makerere in 1940. He arrived in Dar es Salaam in the same year to serve his internship at Sewa Haji Hospital (now Muhimbili National Hospital). His work there was highly regarded and in 1942 he performed the hospital's first major all-African operation.

In April 1942, Mutahangarwa was posted in Shanwa, a remote station in Shinyanga with no railway connection nor telegraph service. This appointment made him the first African Assistant Medical Officer to be in charge of a station in the Tanganyika territory. He managed the hospital with an entirely African Staff. He found however that he had inherited a crisis, an epidemic of cerebrospinal-meningitidis had brocken out during that year. The total number of CSM cases in the following year were in excess of 600 patients and 109 deaths. The CSM epidemic continued through-out his 3.5 year tenure however cases and deaths gradually decreased. A smallpox epidemic erupted in the aread during 1944-1945, and he oversaw the vaccination of 86,604 people in a district with very poor transportation, while at the same time running a 38-bed hospital and an outpatient clinic, and organizing clinical trails of traditional medicines for the treatment of tuberculosis.

Despite Mutahangarwa initial pride and optimism, his years at Shanwa were unhappy. He struggled to manage on his small salary (less than 400 T.Shs a month), was pestered by bureaucrats, drown in paperwork and isolated from other professionals. In 1951 he quit government service and moved to private practise.

Among his contemporaries were the gifted Dr. Francis Mwaisela from Mbeya and Dr. Raymond K

SURGERY IN TANZANIA.

This is a historical survey from 1877 when Tanzania was first introduced to western type scientific medicine by the Church Missionary Society Hospital at Mamboya near Mpwapwa; the arrival of five German military ‘surgeons’ in 1838 at medical headquarters in Bagamoyo; the opening of the Sewa Hadji Hospital in Dar es Salaam in 1883 (following donation of 12 400 rupees by a wealthy Indian merchant of the same name); the first qualified Tanzanian medical practitioner (Joseph R. Mutahangarwa in 1940); and, Tanzania’s own Medical School in 1963.

Madaktari na Siasa Tanganyika

Je unawatambua madaktari hawa na mchango wao kakika kugombea uhuru wa Tanganyika katika miaka ya 1948 - 1950: 
  • Dr Joseph Mutahangarwa
  • Vedasto Kyaruzi
  • Dr Wlibard Mwanjisi
  • Dr Michael Lugazia
  • Dr Luciano Tsere
Mwaka wa 1951 wakati Dossa na wenzake wapo katika juhudi za kuipa uhai mpya TAA Dossa aliandikiwa barua na V.M. Nazerali aliyekuwa mjumbe wa Baraza la Kutunga Sheria akimuomba Dossa aunge mkono juhudi zake na za Ivor Byaldon na Brig. Scupham za kutaka kuunda chama cha siasa kitachowashirikisha watu wa rangi zote. Bayldon na Brig. Scupham walikuwa kama alivyokuwa Nazerali, wajumbe wa Baraza la Kutunga Sheria.
Wanasiasa wengine walioombwa kuunga mkono juhudi hizi walikuwa Dr. Joseph Rutakorezibwa Mutahangarwa wa Kiziba, Chifu Kidaha Makwaia, Liwali Yustino Mponda wa Newala, Chifu Abdieli Shangali wa Machame, Chifu Thomas Marealle wa Marangu, Chifu Adam Sapi Mkwawa, Chifu Harun Msabila Lugusha, Dr. William Mwanjisi, Abdulkarim Karimjee, Dr. Vedas Kyaruzi, Liwali Juma Mwindadi, H.K.Viran, Stephen Mhando, Ally Sykes na Abdulwahid Sykes. Dossa na wenzake waliikataa ghilba hii kwa kuwa lengo lao lilikuwa ni kuanzisha chama cha siasa cha Waafrika wa Tanganyika kwa minajili ya kudai uhuru.
Mwalimu Nyerere alipofika Dar es Salaam kwa mara ya kwanza mwaka wa 1952 kama mwalimu wa shule ya St. Francis' College, Pugu hakuna mtu aliyekuwa anamjua au kupata kusikia habari zake katika ulingo wa siasa. Kassela Bantu ambaye alikuwa akijuana na Nyerere kwa siku nyingi alimchukua Nyerere kwa Abdulwahid Sykes kumtambulisha. Wakati ule Abdulwahid alikuwa Rais wa TAA. Nyerere mara moja akajiunga na baraza la siasa lililokuwa likifanyika Mtaa wa Mbaruku nyumbani kwa Dossa. Ikawa kila Jumapili Nyerere anakuja kutoka Pugu kuja kumtembelea Dossa. Ilikuwa katika baraza hii ndipo Nyerere alipokutana na wanasiasa wengi wa wakati ule kama Ramadhani Mashado Plantan aliyekuwa anamiliki gazeti lililokuwa likijulikana kama Zuhra, John Rupia, Dunstan Omari, Zuberi Mtemvu na wanasiasa wengine. Fikra za Nyerere za kudai uhuru zilisikika kwa mara ya kwanza kupitia kalamu ya Mashado Plantan na gazeti lake la Zuhra lililokuwa likitoka kila siku ya Ijumaa. Fikra za Nyerere ziliingiza msisimko mpya katika baraza lile na haukuchukua muda mwaka 1953 uongozi wa ndani ukampendekeza agombee urais wa TAA.
Dossa anasema ingawa wao kwa kuwa karibu na Nyerere walikuwa wamekiona kipaji chake cha uongozi, wanachama wengi hawakumkubali mara moja na ndiyo maana katika uchaguzi wa TAA uliofanyika Arnautouglo Hall tarehe 17 Aprili, 1953 kati ya Abdulwahid aliyekuwa Rais na Nyerere aliyekuwa anagombea dhidi yake, Nyerere alishinda uchaguzi ule kwa taabu sana. Haukupita muda chama kikaanza kuzorota na mwisho kikafa. Dossa anakumbuka kuwa yeye alikuwa anawapitia viongozi kwenda kwenye mkutano. Akipiga honi ili mtu atoke waende mkutanoni kiongozi alimtuma mkewe atoke nje na aseme kuwa hakuwepo nyumbani.
Dossa anasema ilikuwa baada ya kushauriana na Abdulwahid, Makamu Rais wa TAA ndipo lilipokuja wazo kuwa ni lazima wapate nguvu ya wazee wa Dar es Salaam ili kukifufua chama.Hivi ndivyo TAA katika miaka ya mwisho ya uhai wake ilipokuja kupata kuungwa mkono na wazee wa Dar es Salaam na kupelekea kuundwa kwa Baraza la Wazee wa TANU mwaka 1955 chini ya mwenyekiti wake Sheikh Suleiman Takadir. Nyerere amepata kusema kuwa alikuwa Dossa ndiye aliyemfahamisha aache kuvaa kaptula kwa kuwa sasa atakuwa akitoka mbele ya watu wazima na hiyo si adabu nzuri.
Dossa alikuwa kati ya wale wazalendo watano, Abdulwahid Sykes, Ally Sykes, John Rupia na Julius Nyerere waliokutana ndani ya ofisi ya TAA new Street (sasa Lumumba Street) katika miezi ya mwisho ya 1953 na kwa pamoja wakapitisha azimio la siri la kuibadili TAA kuwa chama cha wazi cha siasa na kukipa chama hicho jukumu la kuiongoza Tanganyika katika kudai uhuru wake. Hili ndilo lililokuwa azimio la kwanza la busara katika historia ya Tanganyika. Azimio la pili la busara ni lile la Tabora la mwaka 1958.
Tarehe 7 Julai, 1954 wazalendo hawa wafuatao wakakutana Dar es Salaam kubadili Katiba ya TAA ili kuanzisha chama cha TANU: Dossa Aziz, Abdulwahid na Ally Sykes, Tewa Said Tewa, Patrick Kunambi, Kasella Bantu, John Rupia, Julius Nyerere, C.O. Millinga,Germano Pacha, Joseph Kimalando, Japhet Kirilo; Abubakar Ilanga, L.M.Bugohe, Saadan Abdu Kandoro, S.M. Kitwana na L.M. Makaranga. Dossa Aziz kadi yake ya TANU ni namba 4 iliyotolewa na kusainiwa na Ally Sykes. Haukupita muda mrefu TANU ikampeleka Nyerere Umoja wa Mataifa. Tarehe 17 Februari, 1955 Nyerere aliondoka Dar es Salaam na kwenda New York kuhutubia Baraza la Udhamini la Umoja wa Mataifa na ndani ya mkoba wake hakuwa na hotuba nyingine ila yale mapendekezo aliyopewa Gavana Edward Twinning mwaka wa 1950 na uongozi wa TAA.Nyerere aliporudi nchini alikuta umati mkubwa wa wananchi unamsubiri uwanja wa ndege. Haikuwezekana kwake kutoka nje ya uwanja jinsi umati wa watu ulivyojazana kumlaki.. Walinzi wa kikoloni walimruhusu Dossa aingize gari yake hadi chini ya mlango wa ndege. Nyerere akashuka na kupokelewa na swahiba wake Dossa na akaingia ndani ya gari la Dossa.
Siku ya pili ulifanyika mkutano mkubwa Mnazi Mmoja ambao gazeti la Zuhra lilikadiria kuwa zaidi ya watu 25,000 walihudhuria. Baada ya mapokezi na mkutano mkubwa, ukafanyika mkutano Mtaa wa Kipata na Sikukuu nyumbani kwa Clement Mohamed Mtamila mkutano ambao ulihudhuriwa na Titi Mohamed, Iddi Faiz Mwafongo, Tatu bint Mzee, Asha Ngoma, Mzee Haidari Mwinyimvua na Nyerere. Katika mkutano huo Nyerere aliwaambia wajumbe kuwa Father Walsh amemuambia ama achague siasa au aendelee kufundisha. Mkutano ukamshauri aache kufundisha ili awe Rais wa chama"Full time" ili kufanikisha wazo hili, Dossa Aziz alijitolea kumlipa mshahara hadi ushindi utakapopatikana.
Ahadi hii aliitimiza.Hizi ndizo zilikuwa harakati za Dossa Aziz. Mzee Dossa akijibu hoja iliyokuwa ikipandikizwa kubadili historia ya kudai uhuru kuwa ati TAA kilikuwa chama cha starehe, Dossa alisema kuwa mtafiti yeyote anaesema kuwa TAA kilikuwa chama cha starehe na aende kwa Nyerere amuulize ikiwa mwaka 1953 alipojiiunga na chama alijiunga kwa minajili ya kujistarehesha au kwa ajili ya siasa. Mzee Dossa alieleza kuwa suala la kupotoshwa kwa historia ya Tanganyiika lilianza kujitokeza mara tu TANU ilipoanza kupata nguvu na viongozi wapya kuingia katika chama hasa baada ya Uchaguzi wa Kura Tatu na akasema kuwa hashangai kuwa leo kuna watu wanabeza juhudi zao na kudai kuwa siasa ilikuja na Nyerere kutoka Butiama.
Urafiki kati ya Dossa na Nyerere ulishamiri kwa kipindi chote cha kudai uhuru na kuja kufifia mara tu uhuru ulipopatikana mwaka 1961. Sababu kubwa ya kukatika kwa urafiki wao ni kuwa kuanzia mwaka 1962 kwa mara ya kwanza nchi ilianza kukumbwa na migogoro ya dini kati ya serikali na Waislamu ambao walihisi kuwa Nyerere alikuwa akifanya njama za kuuhujumu Uislamu kinyume na maadili na ahadi ya TANU. Mwaka wa 1963 Halmashauri Kuu ya TANU ilivunja Baraza la Wazee wa TANU kwa kile kilichodaiwa kuchanganya dini na siasa. Nyerere taratibu aliwahama marafiki zake na wahimili wake wa siku za awali na akaanza kujenga nguvu mpya kutoka kwa wasio Waislamu kwa hofu ya kuwa akiwa karibu na waasisi wa TANU ambao wengi wao walikuwa Waislamu kungehatarisha nguvu zake na nguvu za Kanisa Katoliki. Kuanzia kipindi hiki Nyerere akawa mbali na Dossa na rafiki zake Dossa.
Mwandishi wa makala hii alipomtembea Dossa Aziz nyumbani kwake Aprili, 1987 ilikuwa asubuhi kiasi cha saa nne na alimkuta Mzee Dossa amekaa barazani kwake akiwa amefungulia radio yake akisikiliza BBC. Mara alipotambulishwa kwake alimpokea kwa ukarimu mkubwa. Ukarimu ulikuwa ndani ya damu ya Dossa.
Mbele ya baraza yake yalikuwepo mabaki ya Landrover ambayo Dossa alimfahamisha mwandishi kuwa gari ile aliitumia na Nyerere katika safari za kutembelea majimbo ya Tanganyika kwa niaba ya TANU wakati wa kudai uhuru. Mzee Dossa akionyesha kidole mabaki ya gari yake alisema, "Gari hii imetembea sehemu nyingi sana nikimpeleka Nyerere sehemu tofauti za Tanganyika na katika siku za mwanzo mimi mwenyewe ndiye nilikuwa nikiiendesha gari hii hadi pale tulipomwajiri Said Kamtawa kama dereva wa TANU." Hata kwa wakati ule Mzee Dossa alionyesha dalili zote za kupigwa na maisha. Katika picha ya pamoja ya waasisi wa TANU kuna watu wawili tu ambao wanaonekana wamevaa suti na tai, hao ni Abdulwahid Sykes na Dossa Aziz. Ishara tosha ya hadhi zao. Waliobaki wote wamejivalia mavazi yao ya kawaida. Nyerere akiwa amevaa kaptula na soksi ndefu zilizogota magotini, mavazi maarufu wakati ule kwa wasomi. Picha hii imebeba maneno elfu moja. Dossa aliyeonekana pale kibarazani Mlandizi si yule aliyekuwa kwenye picha ya waasisi wa TANU. Dossa mtanashati, mtoto wa Mwafrika tajiri, Aziz Ali, Waziri Dossa Aziz aliyetoa mali kuipa TANU ili Nyerere aitumie katika shughuli za kuikomboa nchi alikuwa amechoka akionyesha dalili zote za kusahauliwa na nchi aliyoipigania ijitawale.
Tarehe 27 Aprili, 1985, Julius Kambarage Nyerere, sasa akijulikana kwa jina jipya la Baba wa Taifa, katika viwanja vya Ikulu alitoa jumla ya medali 3,979 kwa Watanzania walioiletea nchi hii maendeleo. Si Dossa wala yeyote aliyetajwa katika kumbukumbu hii ya marehemu Dossa Aziz alikuwa katika hao waliopata heshima hiyo. Lakini baadae kama mtu aliyegutushwa Baba wa Taifa alimkaribisha Dossa Ikulu na kumpa medali katika sherehe fupi.
Kwa muda mrefu sasa kumekuwa na hofu kubwa sana ya wale walioshika madaraka ya kuendesha serikali wakiogopa wananchi kuhusisha uasisi wa TANU na nguvu za siasa za Waislamu walioishi miaka ile. Matokeo yake ni kufutika kwa hisotoria ya wazalendo wengi waliojitolea maisha yao kuupigania uhuru wa Tanganyika. Dossa Aziz ni kati ya wazalendo ambao historia imedhulumu haki zao za kutambulika kama mashujaa wa uhuru wa Tanganyika. Kwa kipindi cha zaidi ya miaka thelathini si CCM wala si rafiki yake mpenzi Julius Nyerere alikuwa anafahamu Dossa anaishi vipi na ana hali gani. Rafiki zake wachache waliokuwa wakimtembelea nyumbani kwake pale Mlandizi walihuzunishwa na hali yake. Dossa mtu aliyekuwa na mali katika miaka ya 1950 alikuwa akiishi katika hali ya ufukara. Hali hii ya ufukara ilitaka kumkosesha kuhudhuria Mkutano Mkuu wa CCM mwaka1987 pale Kizota ambapo waasisi wote wa TANU walialikwa. Sababu kubwa ilikuwa ni ukosefu wa nguo na viatu vya kuvaa katika hadhara kama hiyo. Ilikuwa mmoja wa marafiki zake wa zamani (jina ninalihifadhi) ndie aliyemnunulia nguo na viatu vya kumwezesha kwenda Dodoma. Rafiki zake walipomshauri aende kwa Nyerere ampatie msaada Dossa alijibu kuwa yeye hawezi kulifanya hilo kwa kuwa Nyerere anajua kuwa yeye alitumia fedha zake nyingi katika harakati za kudai uhuru na kama yeye Nyerere leo kamsahau yeye hana sababu ya kumfuata. Jibu la Dossa lilikuwa jibu la muungwana, mtu asiyekubali kujidhalilisha.
Kauli hii ya Dossa na msimamo wake huu thabiti ulithibitishwa na Mwalimu Nyerere mwenyewe siku ya Jum apili tarehe 19/4/98 katika khitma ya marehemu nyumbani kwa Dossa pale Mlandizi wakati Nyerere aliposimama kusema machache katika hadhara ile kuhusu uhusiano wake na Dossa na mchango mkubwa wa Marehemu Dossa Aziz katika kuleta uhuru wa Tanganyika.
Nyerere alisema kuwa hata siku moja Dossa hakupata kumuomba kazi au kuonyesha dalili za kutaka ukubwa. Mwalimu Nyerere aliposema maneno haya alibubujikwa na machozi na waliokuwepo nao walilia kwa huzuni.Subira aliyokuwanayo Dossa ndiyo sababu kubwa iliyomfanya astahamili dhiki kwa miaka yake ya mwisho ya uhai wake na afe masikini katika hospitali ya Tumbi, Kibaha badala ya St. Thomas Hospital, London, Dossa hakuwa wa kwanza kukutwa na haya. Haya yalimkuta Mzee Mshume Kiyate, Sheikh Mohamed Ramia na wengine wengi. Baada ya kuleta uhuru wazalendo hao wakageuzwa ganda la muwa. Hakuna unachoweza kufanya na ganda la muwa ulilolifyonza ila kulitema tu na kama utaweza kuelekeza mdomo wako kwenye jalala na kutembea humo hivyo ni bora zaidi kwani hata kulitema ganda hilo kwenye mkono wako wa kushoto kisha kulitupa jalalani ni kulipa hadhi ganda hilo. Habari za Dosa Aziz zinahitaji utafiti wa kina wa msomi makini. Hii ni changa moto kwa wana historia, wana historia wa Tanzania ya leo. Ni katika kuijua historia ya uhuru wa nchi hii ndipo wenye madaraka hivi sasa wanaweza kujua kwa nini hii leo wajukuu wa akina Dossa wameiona dhulma na wanapambana na polisi na as kari wa kuzuia fujo kwa mawe kisha wanachoma moto ofisi za chama ambacho asili yake ni babu zao. 

Baada ya vita kuu ya pili (1938-1945) nchi nyingi zilizokuwa chini ya ukoloni hasa barani Afrika zilianzisha harakati za kudai uhuru.
Uongozi uliokuwepo Tanganyika wa chama cha Waafrika kilichojulikana kama African Association wakati ule ulishindwa kabisa kubuni mbinu mpya za kupambana na utawala wa kigeni.
Ili Tanganyika iende mbele ilikuwa ni lazima uongozi ule uondolewe madarakani. Sababu kuu za kuung’oa madarakani uongozi ni kule kushindwa kwake kupambana na mabadiliko ya siasa yaliyokuwa yakitokea dunia nzima.
Harakati za Waziri Dossa Aziz na kuweka wazi mali yake ili kupambana na dhuluma za Serikali ya Kiingereza katika Tanganyika zinaanza wakati huu. Dossa wakati ule alikuwa kijana mdogo wa miaka 25.
Ili aweze kupata picha halisi ya siasa katika mji wa Dar es Salaam ni lazima msomaji afahamishwe hali iliyokuwepo Dar es Salaam katika miaka ya 1950.
Katika mji wa Dar es Salaam ya miaka 1950 kulikuwa na koo mbili maarufu. Ukoo wa Azizi Ali baba yake Dossa, Ramadhani na Hamza Azizi na ukoo wa Kleist Sykes baba yao Abdul-wahid (1924-1968), Ally na Abbas Sykes.
Wazee hawa wawili walikuwa marafiki na urafiki huu ulienea hadi kwa watoto wao. Watoto wao wakafanya mengi pamoja katika harakati za kudai uhuru wa Tanganyika; na ndiyo maana haiwezekani ikaelezwa habari za Dossa bila kugusa habari za akina Sykes.
Halikadhalika haiwezekani yakaandikwa maisha ya Nyerere au historia ya uhuru wa Tanganyika na mwandishi akapuuza mchango wa watu hawa. Watoto wa koo mbili hizi, Dossa akiwakilisha ukoo wa Azizi Ally na Abdulwahid na Ally Sykes wakiwakilisha ukoo wa Sykes ndiyo mwaka 1950 waliohusika na mapinduzi ya kuung’oa madarakani uongozi wa African Association wa wazee uliodumu kuanzia mwaka 1929 hadi 1950 rais wake wa mwisho akiwa Mwalimu Thomas Sauti Plantan.
Muhimu katika mazingira ya siasa za wakati ule ni kuwa hakuna chochote ambacho kingeliweza kufanyika Dar es Salaam katika jitihada ya kupambana na Serikali ya kikoloni bila ya msaada wa Dossa na watoto wa Kleist Sykes kwa sababu hawa walikuwa kwanza na elimu ya kutosha na pili walikuwa na hazina ya kuendesha harakati za siasa.
Kleist Sykes (1894-1949) alikuwa mwajiriwa wa Tanganyika Railway kama mhasibu. Kleist alikuwa mwanasiasa muasisi wa African Association (1929) na Al Jamiatul Islamiyya (Muslim Association) (1933) katika miaka ya mwisho ya uhai wake Kleist akawa mfanyabiashara maarufu.
Azizi Ally alikuwa mkandarasi wa kujenga majumba. Lakini kwa kuwa Azizi Ali alikuwa Mwafrika wakoloni walimbagua wakakataa kumpa leseni ya ukandarasi wa daraja la juu ambayo ingelimwezesha kujenga majumba makubwa ya ghorofa. Leseni hizo walipewa Wahindi na Wazungu. Juu ya ubaguzi huu wote baba yake Dossa alifanya kazi ya ujenzi na akatajirika katika biashara kama alivyotajirika rafiki yake Kleist. Mali hii ndiyo iliyokuja kuwa mtaji wa kwanza waliotumia Waafrika wa Tanganyika katika miaka ya mwanzo kuanzia harakati za kudai uhuru.
Wakati ule mtu hakujiingiza katika siasa ili anufaike binafsi. Nafasi hiyo haikuwepo kwa kuwa hakukuwa na fedha katika siasa. Kila aliyeingia katika harakati aliingia kwa uchungu na mapenzi ya nchi. Kama alikuwa na mali basi aliingia ili atoe mali yake kuikomboa nchi. Kama hana mali basi alijitolea chochote katika vipawa alivyojaaliwa.
Dossa aliingia katika harakati za siasa mwaka 1950 siasa ikiwa katika hali hii. Aliingia katika African Association na uongozi mpya wa vijana miongoni mwao akiwa Abdulwahid na Ally Sykes, Hamza Mwapachu (1918-1962), Tewa Said Tewa (1924-1998), Dk. Vedast Kyaruzi, Dk. William Mwanjisi, Dk. Luciano Tsere, na vijana wengine ambao ingawa hawakuwa Watanganyika walishiriki kikamilifu katika harakati za kudai uhuru. Hawa walikuwa Dennis Phombeah kijana wa Kinyasa kutoka Nyasaland (Malawi), Patrick Aoko na Dome Budohi kutoka Kenya na vijana wengine wengi.
Dossa aliguswa na madhila ya ukoloni kwa dhahiri yake mwaka 1947. Dossa pamoja na mtoto mmoja wa Mwarabu tajiri aliyekuwa akiishi Dar es Salaam, Ali Mmanga walichaguliwa kuhudhuria mahojiano Nairobi kwa ajili ya kozi ya urubani wa ndege. Walipowasili Nairobi wakoloni walikataa kumfanyia usaili Dossa kwa sababu alikuwa Mwafrika. Dossa alifahamishwa kuwa yeye kama Mwafrika hastahili kupewa ujuzi wa kurusha ndege. Dossa alifadhahika sana na alimweleza mwandishi wa makala hii kuwa alipiga simu kwa baba yake na akawa analia machozi kwa uchungu. Kwa kumuonea huruma baba yake alimtumia fedha ili anunue gari pale Nairobi kama zawadi ya kumfajiri. Hii ndiyo ilikuwa gari ya kwanza kuwa nayo Dossa na aliitumia hadi 1955 alipoitoa kwa TANU ili itumike kwa ajili ya kudai uhuru.
Lakini Dossa alipokwenda Nairobi alimkuta Ally Sykes yupo mjini hapo na tayari alikuwa akifahamiana na wanaharakati wa Kenya kama Jomo Kenyatta, W.W. Awori, Tom Mboya na wengineo. Ally alikuwa akihudhuria mikutano ya siasa ya Wakikuyu iliyokuwa ikifanyika kwa siri Limuru.
Ally Sykes alimchukua Dossa katika moja ya mikutano ya hadhara ambao Kenyatta alikuwa anahutubia katikati ya Nairobi sehemu moja ijulikanyo kama River Road. Aliyoyaona pale yalimtosheleza kabisa Dossa kujua kuwa Tanganyika ilikuwa imechelewa katika harakati za kudai haki yake. Waafrika wa Kenya walikuwa wamefikia hali ya kuzungumza siasa kwenye majukwaa wakati Waafrika wa Tanganyika walikuwa bado wakifanya mikutano yao ndani ya kiofisi kile kidogo cha African Association chini ya uongozi dhaifu wa Thomas Plantan akiwa kama Rais na Clemet Mtamila kama Katibu. Dossa alifikisha yote aliyoyaona Kenya kwa wenzake.
Mzee Dossa alimfahamisha mwandishi wa makala hii kuwa ni katika kipindi hiki kati ya mwaka 1947-1950 ndipo njama za kupindua uongozi wa Africa Association zilipoanza washiriki wakuu wakiwa yeye mwenyewe Dossa, Abdulwahid na mdogo wake Ally na rafiki yao Hamza Kibwana Mwapachu. Huku akicheka Mzee Dossa alimfahamisha mwandishi kuwa:
"Ilikuwa kutokea Tanga Club, Club mahsusi ya vijana wasomi Waafrika iliyokuwepo New Street (hivi sasa Lumumba Str.) si mbali sana na ofisi ya African Association ndipo Abdulwahid na Hamza Mwapachu walipoivamia kwa nguvu ofisi ya African Association na kufanya mapigano ambayo yalimfanya Katibu Mzee Mtamila apigwe na kutupwa nje ya ofisi".
Dossa anasema yeye ingawa alikuwa anauchukia ule uongozi wa wazee hakuwa na moyo wa kuwatoa wazee wale kwa nguvu na kwa taadhira, kwa ajili hii basi alibaki nje akawa anaangalia sakata ile kwa mbali. Uchaguzi ulifanyika na wazee wakang’olewa madarakani. Dk. Kyaruzi akachaguliwa Rais na Abdulwahid akiwa Katibu wake.
Kuanzia wakati huu mikutano ya siasa ikaanza kufanyika Ilala Commuity Centre ambako Hamza Mwapachu alikuwa akifanya kazi kama Assistant Welfare Officer. Nyakati za jioni mijadala hii ikawa inahamia nyumbani kwa Dossa Mtaa wa Mbaruku Gerezani au Tanga Club, Agenda kuu ikiwa namna ya kuwaunganisha Watanganyika chini ya chama cha siasa ili kudai uhuru.
Mwaka wa 1950 Gavana Edward Twining alipoteua Kamati ya Katiba (Consitutional Development Committee) ili kukusanya mapendekezo ya Waafrika ni vipi wangependa katiba ya nchi iwe, Dossa alisema kuwa hapo ndipo Waingereza walipopata kwa mara ya kwanza kuhisi kuwa uongozi mpya wa vijana katika African Association ulikuwa umepania kuleta mabadiliko katika nchi. Uongozi wa akina Dossa uliihimiza Serikali ya kikoloni kuhusu umuhimu wa kuwa na uwakilishi wa Waafrika katika Baraza la Kutunga Sheria, uwakilishi wa kuchaguliwa na wananchi wenyewe badala ya ule uwakilishi wa kuchaguliwa na Gavana rangi ya mtu zaidi kuliko sifa nyingine yoyote.
Kipindi hiki cha mwaka 1950-1954 kilikuwa kipindi kigumu sana kwa kuwa kwanza chama kilikuwa hakina fedha kikitegemea sana msaada wa Dossa. Wakati ule chama kilitegemea sana fedha za Dossa katika shughuli za kuendesha ofisi na gari yake katika kutimiza majukumu yake ya kila siku.
Kwa kipindi kirefu wakati wa uongozi wa wazee kulikuwa hakuna mawasiliano yoyote kati ya Waafrika wa Tanganyika kupitia African Association na Baraza la Udhamini la Umoja wa Mataifa ambalo ndilo lililokabidhi Tanganyika kwa Waingereza wailee nchi hadi hapo Waafrika watakapokuwa tayari kujitawala. Kwa bahati mbaya Waingereza hawakutoa umuhimu wowote katika kuwafahamisha Waafrika mapatano hayo kati yake na Umoja wa Mataifa. Vijana walichukua nukta hii kama kazi ya kwanza kwa umuhimu katika chama na walipeleka barua nyingi sana katika matawi ili kuyaamsha kwa kuwa yalikuwa yamelala kwa muda mrefu.
Kati ya mwaka 1950-1952 Dossa alishiriki katika mikutano kati ya TAA na Earle Seatonn mwanasheria kutoka Bermuda aliyekuwa akikishauri chama katika masuala mbali mbali ya Katiba na sheria, kutayarisha mapendekezo kwa Constitutional Developmet Committee na katika mgogoro wa ardhi ya Wameru.
Vile vile Dossa alishiriki katika kutuma ujumbe wa TAA ulioongozwa na Abdulwahidi kwenda Kenya ambao ulikutana na uongozi wa KANU wa Jomo Kenyatta, Fred Kubai, Bildad Kaggia na Kungu Karumba mwaka 1951.
Halikadhalika Dossa alikuwa mjumbe wa TAA uliokuwa ukutane tena na Kenyatta kwa mazungumzo ya siri Arusha mazugumzo yaliyoombwa na KANU. Wajumbe wengine wakiwa Abdulwahid na Stephen Mhando.
Katika salaam alizoleta Kenyatta kwa TAA alihimiza kuwa kila mjumbe wa TAA asije mkutanoni ila awe amebeba silaha. Ujumbe huu ulikuwa uondoke kwa siri mmoja mmoja ili kukwepa makachero.
Dossa alikuwa wa kwanza kuondoka kuelekea Arusha akiwa na bunduki. Wakati ule ili kwenda Arusha njia ilipita Dodoma. Mkutano huu haukufanyika kwa kuwa Kenyatta na wenzake walikamatwa kwa makosa ya kuwa wafuasi wa Mau Mau.
Akiwa Dodoma Dossa alifahamishwa na Ali Juma Ponda katibu wa TAA Dodoma kuwa mkutano hautakuwepo kwa kuwa viongozi wa KANU wote wametiwa mbaroni. Akiwa njiani kwenda Arusha palitokea mapigano kati ya Mau Mau na askari wa kikoloni.
Tarehe 20 Oktoba, 1952 serikali ya kikoloni Kenya ilikuwa imeshindwa kabisa kupambana na Mau Mau, kwa sababu hii basi serikali ilitangaza hali ya hatari, Kenyata na Uongozi mzima wa KANU ukatiwa kizuizini ( tarehe 8 Aprili 1953)wakahukumiwa kifungo cha miaka saba kazi ngumu). Dossa aliamua kwenda Mwanza ambako alipokewa na Dk. Joseph Mutahangarwa, Makamo wa Rais wa TAA Lake Province. Dk. Mutahangarwa aliulaumu uongozi wa Makao Makuu kwa kuunganisha harakati za TAA na KANU kwa hofu ya kusababisha kamata kamata kama ile iliyokuwa ikiendelea Kenya.
Dossa Azizi alikwenda Bukoba ambako alipokelewa na Chief Rutinwa wa Kiziba na viongozi wengine wa TAA kama Ali Migeyo na Suedi Kagasheki.
Mwaka 1953 Dossa alihusika na uamuzi wa kuupeleka ujumbe wa TAA wa Saadan Abdu Kandoro, Japhet Kirilo na Abbas Sykes utembee nchi nzima kuwaeleza wananchi kile kilichopitika Umoja wa Mataifa kuhusu kesi ya ardhi ya Wameru. Vile vile katika mwaka huo huo Dossa alihusika katika uamuzi wa kuupeleka ujumbe wa TAA Southen Rhodesia (Zambia) kuhudhuria mkutano uliojulikana kama Pan African Congress uliotayarishwa na mwanasiasa mmoja aliyeitwa David Keneth Kaunda aliyekuwa Katibu wa African National Congress. Wajumbe waliochaguliwa kuiwakilisha TAA katika mkutano huu walikuwa Ally Sykes na Denis Phombeah. Katika harakati hizi zote zilipotakikana fedha kwa ajili ya kufanikisha hili au lile jukumu lilimwangukia Dossa. Dossa alitoa fedha zake kwa ukarimu na bila kinyongo.
Mwaka wa 1951 wakati Dossa na wenzake wako katika juhudi za kuipa uhai mpya TAA Dossa aliandikiwa barua na V.M. Nazerali aliyekuwa mjumbe wa Baraza la Kutunga Sheria akimuomba aunge mkono juhudi zake na za Ivor Bayldon na Brig. Scupham za kutaka kuunda chama cha siasa kitachowashirikisha watu wa rangi zote. Bayldon na Birg. Scupham walikuwa kama alivyokuwa Nazerali, wajumbe wa Baraza la kutunga sheria.
Wanasiasa wengine walioombwa kuunga mkono juhudi hizi walikuwa  Dk. Joseph Mutahangarwa, Chifu Kidaha Makwaia. Liwali Yastio Mponda wa Newala. Chifu Abdieli Shangali wa Machame, Chifu Thomas Marealle wa Marangu, Chifu Adamu Sapi Mkwawa, Chifu Haru Msabila Lugusha, Dk. Wiliam Mwanjisi, Abdulkarim Karimjee, Dk. Vedast Kyaruzi, Liwali Juma Mwindadi, H.K. Viran, Stephen Mhando, Ally Sykes na Abdulwahid Sykes.
Dossa na wenzake waliikataa ghilba hii kwa kuwa lengo lao lilikuwa ni kuanzisha chama cha siasa cha Waafrika wa Tanganyika kwa minajili ya kudai uhuru.

11 comments:

Anonymous said...

I love reading through an article that can make men and women think.
Also, thanks for allowing for me to comment!

my homepage - external hemorrhoids treatment

Anonymous said...

As a Professional Wedding Decorator, I am here to help take away some of the stress involved in decorating for your wedding and cleaning up afterwards.

Tape the center point of the ribbon onto a table to make it easier to manipulate the ribbon.
This theme could also extend to the wedding bouquet and the bridesmaids could wear simple daisy headdresses.

Also visit my web site :: Here are some Weddin

Anonymous said...

Weight loss does not involve exercising only. Some people
may be concerned that if they are getting the subliminal messages through hypnosis that other suggestions could be entered as well.
Using different products along with body by vi, life transforming health benefits are enjoyed along with weight
loss and other fitness regimes.

Also visit my web page: loosing weight

Anonymous said...

This info is priceless. When can I find out
more?

my homepage; does quantrim really work

Anonymous said...

These are powder coated to make them rust free and then given different
finishes. Most of the people know the decorations in their
living room or in the house. Why not then consider cheap garden decor
ideas such as turning to eco-friendly solutions such as solar garden decor.

Here is my page; river rock garden ideas

Anonymous said...

As a result, you want to choose a fall wedding cake design that will develop your theme.
You can go in for combination of one favorite color of the bride and groom for the cake.
Wherever your creativity leads you one can.

My web site ... http://www.cakedecoratingtrends.com/

Anonymous said...

The time saved will all depend on just how much decorating you prepare on undertaking.
For most people, Christmas decorating ideas are frequently minimal to decorating the
tree along with the lounge and making the dining-room table appear magnificent.
Think of a Christmas decorating tips employing more compact boughs and greenery currently being the centerpiece on
your dining space table.

Look at my blog post; pictures of exterior christmas decorations

Anonymous said...

Even if a full course meal is not on the menu, coffee, dessert, and drinks are made more appetizing when you sit down to a well dressed
table. Keeping it Consistent Any good kitchen theme
is only as good as its decor design. It also adds a pop of color and livens up the
dining table.

Feel free to visit my page :: Modern Computer Table Design

Anonymous said...

That they like to decorate the room from the barbie
and consequently that prefer to have a space similar to
the barbie's room. For those persons who has no interest in tile, you should not merely actively communicate with designers, construction teams, but in addition get some understanding on tiles. Use your mantle, a wall shelf, of even your coffee table to show an assortment of cheap Halloween figurines.

Feel free to surf to my homepage; country dining room decor

Anonymous said...

right here replica gucci bags important source check this site out visit our website look these up

Anonymous said...

lien sacs répliques acheter en ligne cliquez pour lire dolabuy hermes site Web ici Chrome-Hearts Dolabuy